Ubelgiji yatoa mbinu ilivyoimaliza Brazil robo fainali Kombe la Dunia

Wakati Roberto Martinez, akieleza Ubelgiji ilibidi kubadili mfumo wao ambao uliwanufaisha kimbinu na kuweza kuwashika vilivyo Neymar na Philippe Coutinho, hivyo kufanikiwa kushinda na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia, kiungo wa timu hiyo, Youri Tielemans, amesema kocha huyo iliwanoa kwa kuwakwepa waandishi wa habari kuepuka siri kuvuja.

 

belgium

“Wakati unapocheza dhidi ya Brazil unapaswa kuwa na faida ya kimbinu. Itakuwa ni rahisi sana kuwa na matumaini, mambo yatakwenda upande wako na kushinda mechi. Lakini sikudhani kama hilo litatokea dhidi ya Brazil,” Martinez aliumbia mkutano wa wanahabari.

“Waliingia na saikolojia hiyo. Unapocheza dhidi ya Brazil unacheza dhidi ya jezi ya njano, ambayo imetwaa Kombe la Dunia mara tano na unapaswa kuwa imara kimbinu.

Ilikuwa ni bahati na siku kubwa kwa sababu kubadili mbinu katika Kombe la Dunia, inamaana wachezaji wanapaswa kuamini.

“Ilikuwa wazi kabisa kutofunguka na kuzuia, tulipaswa kuzima mashambulizi ya Neymar na [Philippe] Coutinho, kuzunguka na kasi ya Paulinho, kurejea kwa Marcelo na kasi ya mmoja kwa mmoja kutoka kwa Willian. Kulikuwa na mashambulizi mengi ya kuyazima.

“Lakini tulipaswa kuwa na mashambulizi yetu kutoka kwa Eden [Hazard] na Romelu [Lukaku] walituwezesha hilo kutokana na kujipanga kwao.

KDB

Hata hivyo, Tielemans, alisema Martinez alisubiri hadi waandishi wa habari walipoondoka kabla ya kuanza kutoa mbinu kwa safu ya ulinzi mahususi kwa ajili ya kuimaliza Brazil ambayo tuliichapa 2-1.

“Ukweli tulizungumza pamoja,” alisema Tielemans. “Tulikuwa na awamu mbili za mazoezi ambapo tulifanyia kazi mbinu hizo pindi tu waandishi walipoondoka.

“Samahani, lakini hiyo ni namna pekee ambayo tunaweza kufanya kazi.”

Beki huyo mwenye umri wa miaka 21, anayeichezea Monaco, alisema kukutana na Ufaransa hatua ya nusu fainali itakuwa ya kipekee kwa upande wake binafsi.

Pia aliwaonya wachezaji wenzake kuelekea changamoto iliyopo mbele yao, akiongeza: “Tunatumai tutasonga mbele dhidi ya Ufaransa katika mechi ijayo. Itakuwa juu yetu kuifanya kazi yetu ila itakuwa ni vigumu sana.

“Hawa ni majirani zetu. Kila mmoja anawajua vizuri Ufaransa. Wanayo timu nzuri sana na historia kubwa.

“Kwangu mimi itakuwa ya kipekee zaidi. Kwa upande wa kimpira, mimi ni Mfaransa. Lakini tutapaswa kupuuza yote hayo na kufanya kama tulivyofanya dhidi ya Brazil.”

Hivyo sasa, Ubelgiji itavaana na Ufaransa katika Uwanja wa St Petersburg kesho Jumanne.

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s