#WorldCup2018: Neymar, Firmino waibeba Brazil hadi robo fainali, Ubelgiji “chupuchupu”

Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea hatua ya robo fainali za kombe la dunia nchini Urusi, hadi hivi sasa tayari timu sita (6) zimefuzu kuingia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, tukisubiri michezo miwili ya leo Jumanne na kupita kwa timu (2) ili kukamilisha idadi ya timu nane (8) katika hatua hiyo.

Timu zilizoingia robo fainali jana Jumatatu

Brazil

01

Mabao ya Neymar na Roberto Firmino yametosha kuibeba Brazil hadi robo fainali wakiichapa Mexico 2-0 katika mchezo wa jana uliofanyika Samara, Urusi.

Brazil ilitafuta njia yake yenyewe ya kusonga mbele dhidi ya wapinzani wake hao wa Amerika ya Kati, kwa kucheza soka la malengo na kufanikiwa kupata ushindi huo muhimu.

Kipigo hicho ni habari mbaya kwa Mexico ambayo kwa mara nyingine wametolewa katika hatua 16 ya Kombe la Dunia ikiwa tangu 1994 wameshindwa kuvuka hatua hiyo.

Katika mchezo huo wa jana, Mexico walitengeneza nafasi nyingi, lakini hali ilibadilika na kuwaacha Brazil na Neymar kuanza kutawala mchezo huo.

Ubeligji (Belgium)

02

Timu ya taifa ya Ubeligji nayo imefanikiwa kutokea nyuma kwa mabao 2 na kushinda kwa 3-2, mchezo wake wa raundi ya 16 bora dhidi ya Japan uliomalizika usiku wa jana huko mjini Rostov, Urusi.

Ubeligji imevunja rekodi ya Ujerumani ya mwaka 1970 ambapo ilitoka nyuma kwa mabao 2 na kushinda dhidi ya England lakini wao wakishinda ndani ya dakika 120 lakini Ubeligji wameshinda ndani ya dakika 90.

Mabao ya Japan ambayo yaliwashangaza wengi, yalifungwa kwa haraka haraka kipindi cha pili kupitia kwa Genki Haraguchi dakika ya 48 na Takashi Inui dakika ya 52.

Ubeligji walisawazisha kupitia kwa Jan Vertonghen dakika ya 69 na Marouane Fellaini dakika ya 72 kabla ya Nacer Chadli kufunga bao la 3 dakika ya 90.

Ubeligji sasa watakutana na mabingwa mara 5 wa Kombe la Dunia Brazil katika hatua ya robo fainali.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s