Mikataba yakibabe inayomfanya Ronaldo kuwa mwanamichezo tajiri zaidi duniani

Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ndio mwana michezo mwenye mvuto zaidi wa kibiashara kuliko yoyote duniani kutokana na deals nyingi za kibiashara alizonazo nahodha huyo wa Ureno, Imeelezwa.

cristiano-ronaldo-eibar_1vt81fq2bcvkp1duhqhoich5by

Kiujumla nyota huyo ana mikataba 31 na makampuni ya biashara duniani, mikataba hii inamfanya kuwa mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi zaidi katika ulimwengu.

Haijalishi ni sekta ipi, brands kubwa duniani zinapenda kujihusisha na mwanasoka huyu. Makampuni kutoka kaskazini mwa Afrika, Marekani, Japan, Ulaya na kwingine kote utamkuta CR7.

Ingawa hakuna namba rasmi ya mikataba yake mingine lakini mkataba mkubwa kabisa wa Ronaldo unaripotiwa kuwa mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike, kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Verdict.

Ronaldo anaingiza benki kiasi cha paundi millioni 21 sawa na zaidi ya billioni 75 kwa mwaka, inaelezwa kuwa mkataba huo anao kwa maisha yake yote, anaungana na wacheza kikapu kama Lebron James na Michael Jordan kuwa watu pekee wenye mikataba ya maisha na Nike.

Ronaldo Jordan

Hapa nimekuelezea baadhi ya Makampuni (03) yenye mikataba katika matangazo yake ya biashara na Ronaldo ambayo imewekwa wazi mitandaoni.

Kampuni ya kiingereza ya Castrol

Castrol ni kampuni ya kiingereza inayojihusishi na utengenezaji wa mafuta, vilainishi, oils za magari, na vifaa vingine vya moto. Hii ni kampuni nyingine ambayo imemtumia na inaendelea kumtumia Ronaldo katika matangazo yake ya biashara.

Mwaka 2009 alisaini nao mkataba wa miaka 2 uliokuwa na thamani ya £8.5m sawa na zaidi ya billioni 25 za kitanzania. Mwaka jana Ronaldo aliongeza tena mkataba wake na Castrol japo taarifa za malipo ya mkataba huo bado hazijatolewa.

Kampuni ya mawasiliano ya ZTE

ZTE ni moja ya kampuni ya mawasiliano inayofanya kazi na Ronaldo na wanaripotiwa kumlipa kiasi cha £3m kwa mwaka (zaidi ya billioni 10 za TZ). Akiwa na miaka 33 akielekea ukingoni mwa maisha yake ya soka, CR7 bado anaonekana kuendelea kuvutia makampuni makubwa.

Kampuni ya Magari ya Toyota

Toyota ni kampuni nyingine iliyojiunga na brand ya CR7 hivi karibuni na dili hili la kampuni hii lina mhakikishia nafasi ya kwanza tena katika listi ya wanamichezo wanaolipwa vizuri zaidi duniani. Forbes waliripoti kwamba kwa mwaka 2017 Cristiano Ronaldo aliingiza bank kiasi cha $93m sawa na zaidi ya billioni 220 za kitanzania.

Jarida hilo liliendelea kuripoti kuwa $58m kutoka kwenye fedha hizo zimetokana na mshahara na bonasi kutoka Real Madrid na nyingine zimetoka na malipo ya udhamini wa makampuni ya biashara na biashara zake nyingine binafsi.

(Data zote kwa msaada wa mtandao wa Sportcal kupitia Verdict)

 ronaldooooo

Orodha ya makampuni yote ya biashara yanayofanya kazi na Ronaldo

(01) Coca Cola, (02) KFC, (03) video games maker Konami, (04) Emirates Airline, (05) Banco Espirito Santo, (06) Castrol Oil & petrol, (07) Emporio Armani, (08) Soccerade Sports drink, (09) Herbalife Supplements & sports nutrition, (10) JBS Clothing (retail)

(11) Samsung Consumer electronics, (12) Jacob and Co. Fashion, (13) TAG Heuer Watches, (14) Clear Shampoo Cosmetics & toiletries, (15) Sportlobster, (16) MTG Pharmaceutical, (17) PokerStars.com, (18) Abbott Laboratories, (19) Altice, (20) ZTE

(21) Smaaash Entertainment, (22) XTrade, (23) Exness Brokerage & consulting, (24) PanzerGlass, (25) Egyptian Steel, (26) American Tourister, (27) Toyota.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s