Jinsi Heineken ilivyonogesha Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League jijini Dar

Ulikuwa ni usiku wenye shamra shamra na msisimko wa aina yake pale ambapo wapenzi wa soka, na watu maarufu walipokutana kwa pamoja Msasani jijini Dar es Salaam kushuhudia fainali za Klabu Bingwa Barani Ulaya kwa mwaka 2018.

Baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wakiongozwa na Jamillah Mwarangi (katikati) wakisherehekea fiaiali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League George & Dragon Bar iliyopo Masaki. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.

Zaidi ya mashabiki 2600 wa Kitanzania, waliweza kufurahia fursa ya kipekee ya kutazama fainali hizo katika mazingira safi ambapo miamba wa soka Liverpool kutoka nchini Uingereza walikutana na miamba wa Hispania Real Madrid. Katika mtanange huo Real Madrid .walitawazwa mabingwa baada ya kuwalaza Liverpool .kwa mabao 3 – 1.

Shabiki wa Real Madrid Roseema Maro akihohiwa na Jimmy Kabwe baada ya ushindi wa fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken

Ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu na inayotizamwa na mamilioni ya watu kote duniani, Heineken iliweza kuwaleta pamoja Watanzania chini ya bia yao pendwa ya Heineken na kupata fursa ya kutazama fainali hizo.

Meneja wa Heineken Afrika Mashariki Njeri Mburu alisema, “Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni moja kati ya ligi zinazohusisha wachezaji wakubwa. Timu zote bora barani Ulaya zinashiriki ligi hii. Kwa uapnde mwingine, bia ya Heineken ni bia inayojulikana na kutumiwa na watu wengi kote duniani na kwa hiyo kuna uhusiano kati ya Heineken na ligi ya mabingwa. Mwaka huu, wateja wetu siyo tu hawatafurahia kutazama ligi bali pia kushiriki fursa zinazokuja na ligi.”

Baadhi ya washabiki wakisherehekea finali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League George & Dragon Bar iliyopo Masaki. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.

Aliongeza “Bia ya Heineken inatengeneza msisimko katika ligi hii kubwa duniani kwa kuwaleta pamoja kwa mamna ya pekee ambayo ni Heineken tu wanafanya. Kwa Tanzania, Heineken imetoa haki za kipekee kwa mashabiki kuweza kushirikia katika kutizama fainali katika mazingira tulivu na ya aina yake kwenye maeneo mbali mbali kama Red Sea Arena, George & Dragon na Club 777. Fainali hii pia ilitizamwa katika shehemu tofauti tofauti 8 katika shehemu mbali mbali nchini,”

Njeri aliongeza kuwa, wateja wa Heineken waliweza kushiriki pamoja na kubadilishana taarifa za matukio wakati wakitazama fainali kupitia kibwagizo #ShareTheDrama. “Tunafurahi kuwa bia ya Heineken ni bia ya Watanzania na siku zote wamekuwa sehemu ya kile tunachokifanya na hata wanam kunywa zaidi bia yetu,” aliongeza. Alisema ikiwa kama bia yenye jina kubwa, siku zote imekuwa ikidhamini na kuwekeza kwenye michezo ambayo inayowagusa wateja wake na kuwaleta pamoja katika masoko yanayochipukia kama Tanzania.

Wakati wa fainali hizo, Heineken iliwazawadia wateja wake bidhaa mbali mbali zi zinazotokana na ligi hiyo. Taarifa zinapatikana kwenye http://www.facebook.com/Heineken na Twitter https://twitter.com/Heineken_TZ

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s