Fahamu haya juu ya kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery

Jina la Unai Emery limeibuka kuwa chaguo la kwanza kwa mabosi wa Arsenal na kuthibitishwa kuteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye amestaafu baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 22. Habari za Mikel Arteta achana nazo tena.

maxresdefault

Tetesi za kocha huyo kutua Arsenal, zilianza kuvuja tangu jana na sasa uongozi wa klabu hiyo umethibitisha rasmi. Mtandao rasmi wa klabu ya Arsenal uliweka taarifa hiyo leo Jumatano ikisomeka kuwa, “Unai Emery ndiye amekuwa kocha wetu mpya”.

Hata hivyo, Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis amesema kocha huyo amekuwa na rekodi bora katika kazi yake na ana mtindo mzuri wa uchezaji mpira utakaoifaa Arsenal.

Emery mwenye umri wa miaka 46 amejiunga na Arsenal baada ya kuondoka Paris Saint-Germain (PSG) huku akiwa ameitumikia kwa takribani miaka miwili ambapo pia aliingoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa League 1.

Unai kutua Emirates akiwa na rekodi ya kuiongoza PSG kumaliza msimu na mataji manne nchini Ufaransa.

Mashabiki wa Arsenal wanaimani kubwa kuwa huyu ni mtu sahihi wa kurejesha ufalme wao wa mataji, lakini ukweli ni kuwa, wengi hawamjui kiundani bwana mkubwa huyu. #SNS Sport tumekusaidia hilo.

emeryedit

Wasifu wake ukoje?

Emery ni kocha mwenye uzoefu mkubwa akiwa na rekodi ya kufanya kazi katika nchi mbalimbali ikiwemo Hispania, Russia na Ufaransa.

Katika miaka 13 ya ukocha ameongoza mechi 719 akiwa na timu mbalimbali. Ni ngumu sana kumfananisha na Arteta katika upande huo.

Ni mtu anayependa kushinda?

Jibu fupi na rahisi ni ndio. Emery amebeba mataji 10 katika maisha yake ya ukocha. Kwa umri wake wa miaka 46 ni wazi bado atakuwa na tamaa ya kuendelea kushinda zaidi na zaidi.

Wengi wanaweza kubeza mafanikio aliyoyapata akiwa na timu ya PSG na hii ni kwa sababu ya ubora wa kikosi alichokuwa nacho.

Lakini Unai amebeba mataji mawili nchini Ufaransa akiwa na rekodi ya kuwasumbua wapinzani wao AS Monaco.

Achana na hayo ya PSG, ufalme wa Unai ulikuja enzi akiiongoza klabu ya Sevilla, alipofanikiwa kubeba mataji ya Uropa matatu mfululizo (kutoka 2014 hadi 2016.

Alishawahi kucheza mpira?

Ndio, lakini si katika kiwango kikubwa. Emery ametumia maisha yake ya soka kama mchezaji akiwa Hispania katika klabu za Toledo na Racing Ferrol, lakini pia anakumbukwa kwa kuchemka kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Real Sociedad.

Enzi zake alikuwa kiungo, akicheza mechi zaidi ya 300 katika kipindi cha miaka 14 kabla hajaamua kuachana na soka na kuingia kwenye ukocha akiwa na umri wa miaka 33.

Staili yake ni ipi?

Safi, soka lake halifanani na falsafa zilizoachwa na Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal. Unai ni mwalimu tofauti kabisa.

Huyu anapenda kucheza kwa tahadhari, japo ni mzuri katika kutengeneza mbinu za mashambulizi ya kushtukiza.

Mara zote anapenda timu yake ifunge mabao ya kutosha. Kama unakumbuka PSG chini yake iliweka rekodi ya kuwa timu iliyofunga mabao mengi katika hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alishawahi kufeli kwenye ukocha?

Ndio, katika kipindi kifupi alichofanya kazi Russia, Emery alishinda mechi 12 na kufungwa 11 katika michezo 26 aliyofanya kazi kama kocha.

Ni ngumu kusema kuwa kushindwa kuipa PSG taji la Ulaya ni kufeli, lakini tukio la Barca kupindua matokeo ya mabao 4-1, linabaki katika kumbukumbu mbaya za mtaalamu huyu.

Ni mtu sahihi kwa Arsenal?

Emery aliweza kuisimamisha Valencia katika misimu minne aliyofanya kazi katika kikosi hicho.

Licha ya anguko la kiuchumi lililoikumba klabu hiyo, Emery aliingoza Valencia kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa La Liga.

Msimu uliofuata alimaliza katika nafasi ya tatu licha ya uongozi kufanya maamuzi ya kuwauza David Villa na David Silva kwa pamoja.

Hivyo suala la bajeti ndogo si tatizo sana kwa Unai japo katika dunia ya soka hivi sasa, bajeti ya usajili ya pauni mil 50 ni ndogo sana kwa timu inayotaka kupambana na Manchester United, Manchester City, Liverpool na Chelsea.

Mashabiki wa Arsenal ni vyema wakajiandaa kwa yote.

Hakika Arsenal ya Unai Emery itanoga sana!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s