#Road2WorldCup: Fahamu wababe wenye vikosi vya dhahabu Russia

Siku kama haziendi kabisa yaani, na joto la Fainali za Kombe la Dunia linazidi kupanda kiasi ambacho mashabiki kote duniani wanatamani kama ligi zingemalizika hata leo kwa kuwa ligi nyingi barani Ulaya mabingwa wake tayari washajulikana hivyo hakuna jipya sana.

Kuelekea kule Russia, aisee kila timu imejipanga usiambiwe. Hakuna timu inayokwenda kuuza sura ni kazi kazi tu.

1jjfcyxskqc9x5cuqnfunka

Lakini ukiwauliza mashabiki na wadau wengi wa soka kuhusu timu gani ambazo zina ‘vikosi vya dhahabu’ kwa maana ya kikosi cha kwanza kufanana au kukaribiana na ubora wa kikosi chab pili kilicho nje, majibu yake yanadondokea kwa vigogo wafuatao:-

Ufaransa

Katika makocha ambao hawatakuwa na visingizio atakaposhindwa kunyakua ubingwa wa kombe la dunia atakuwa Deschamps. Ana ukwasi wa vikosi viwili vinavyotaka kukaribiana ubora kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji katika zama hizi kama Pogba, Kante, Mbappe, Griezmann, Dembele, nk.

Deschamps alipoteza katika mchezo wa fainali za mashindano ya Ulaya mwaka 2016 dhidi ya Ureno katika ardhi yao, mwaka huu ana mtihani mwingine kule Russia akishindwa kuchanga karata zake vyema basi ataonyeshwa mlango wa kwa heri.

Ujerumani

Hawa wajukuu wa Hitler hawana masihara kabisa, si unakumbuka kile kikosi kilichopelekwa kule Russia kwenye michuano ya Kombe la Mabara na wakabeba ndoo ile? Basi bana hawa majamaa nao pia watakiwasha sana Russia. Wana wigo mpana sana wa vikosi kiasi ambacho wachezaji huonyesha ubora wa hali ya juu kupata namba kikosini.

Bingwa huyu mtetezi bado anapewa nafasi kubwa kutokana na vipaji vingi vya akina Sane, Warner, Muller, Draxler, Kimmich, Gomez na nk.

Hispania

Kikosi cha ‘La Roja’ pia ni miongoni mwa vikosi ambavyo vina mafundi wengi sana. Mpira mwingi ulipigwa na kikosi hiki ambapo walifanikiwa kuwagaragaza Argentina kwa magoli 6-1 kutokana ukali wa washambuliaji ambao waliokuwa wanashindania nafasi katika kikosi hicho kama akina Iago Aspas, Rodrigo Moreno, Diego Costa, Alvaro Morata nk.

Tutegemee mbungi la maana pale Russia huku Hispania wakiwa wanataka kufuta rekodi mbaya ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambapo waliondoshwa katika hatua ya makundi na Uholanzi.

Brazil

Enzi sasa kama vile zimejirudia si unakumbuka miongo kadhaa nyuma enzi za akina Romario, Roberto Carlos, Dunga, Cafu, Rivaldo, Ronaldo, nk. Unaweza sema sasa mafundi hawa wa mpira wamezauliwa upya. Wana kikosi kipana sana kiasi ambacho unaweza ukashangaa mpaka Firmino wa Liverpool anaanzia benchi.

Brazil wanataka kurudisha makali yao ya zamani nin suala la mwalimu kuchanga karata zake vyema kuel Russia.

Ubelgiji

Kikosi cha Ubelgiji kimekuja katika wakati mzuri sana, wakati wa kusaka taji la dunia. Ni miongoni mwa timu zenye ukwasi wa wapambanaji, unazungumzia huduma ya watu kama akina Hazard, Lukaku, Witsel, Dembele, Raja Naingollan, Carrasco, Thomas Meunir, Kevin De Bruyne wakati akina Fellaini wanaweza kuanzia benchi na mechi ikawa nyepesi kwa kikosi hiki.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s