Rasmi: Simba SC yatwaa ubingwa wa VPL 2017/18

Hatimaye Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa mwaka 2017/18 baada ya mabingwa watetezi Yanga kuvuliwa ubingwa huo kufuatia kichapo cha mabao 2-0 ilichopata kutoka kwa Prisons katika mechi ya ligi hiyo iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Sokoine.

simba-bingwa_1525968164-1600x705

Kutokana na matokeo hayo, Simba jana ilitwaa ubingwa ikiwa njiani kuelekea Singida kutokana na kuwa na pointi 65 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hata kama itapoteza mechi zake tatu zilizosaliwa dhidi ya Singida United, Kagera Sugar na Majimaji.

Simba ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Kubashiriki Matokeo Michezoni ya SportPesa sasa rasmi mwakani itashiriki mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuyakosa kwa misimu minne iliyopita, huku watani zao Yanga mwakani hawatashiriki mashindano yoyote ya kimataifa kutokana na kutolewa katika michuano ya Kombe la FA.

Yanga imeendelea kubakia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 48 ikifuatiwa na Prisons ambayo jana imefikisha pointi 44 na nafasi ya tano inashikiliwa na Singida United yenye pointi 41 na kesho itawakaribisha mabingwa wapya kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Namfua.

This is Simba Brother!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s