Yanga wakibugi tu leo, ubingwa VPL kutua msimbazi bila jasho

Wekundu wa Msimbazi Simba SC huenda wakatangaza ubingwa leo endapo Yanga SC watashindwa kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kiporo dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi leo wanashuka kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya kurudiana na Wajelajela hao, mchezo utakaokuwa ‘live’ Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni.

ommmy

Endapo Yanga watapata matokeo ya sare au kufungwa, Simba watachukua ubingwa kama walivyofanya Manchester City ya England baada ya West Brom kuifunga Manchester United ambao ndio waliokuwa wakichelewesha taji hilo kutua Etihad.

Simba kwa sasa ndio vinara wa ligi hiyo, wakiwa wamebakiza pointi mbili tu kutangaza ubingwa na wanaweza wakaupata bila kucheza kama Yanga watakubali kuvutwa shati na maafande hao wa Prisons.

Wakati Yanga wakicheza leo, Simba wanasubiri mpaka Jumamosi ya wiki hii kucheza dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida, lakini wanaweza wakashuka kwenye mchezo huo wakiwa wameshatwaa ubingwa.

Kinachowapa jeuri Simba kwamba huenda safari yao ya ubingwa ikarahisishwa leo, ni kutokana na namna Prisons walivyo na kikosi chenye makali hasa kinapokuwa uwanja wao wa nyumbani.

Yanga fc

Kutokana na hali hiyo, wanaamini kikosi cha Yanga hakina ubavu wa kupata ushindi mbele ya maafande hao na kama watakaza sana, watapata sare ambayo pia itakuwa nafuu kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Habari zinazowezekana kuwa nzuri zaidi kwa watu wa Simba ni kwamba Yanga imetuma kikosi dhaifu Mbeya kuivaa Prisons, huku wakiwaacha nyota wao Dar es Salaam ili kukusanya nguvu za kuwavaa Rayons Sports ya Rwanda, katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba wanaongoza wakiwa na jumla ya pointi 65, Azam FC wakifuata na pointi zao 49, Yanga wakiwa nafasi ya tatu na pointi 48.

Japo Simba wamebakisha michezo mitatu, huku Yanga wakiwa na sita mkononi, wanachotafuta Wekundu wa Msimbazi hao ni pointi mbili tu ili kufikisha pointi 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Lakini iwapo Yanga watafungwa au kupata sare leo, hata kama Simba watapoteza mechi zao zote zilizobaki, huku watani wao hao wakishinda zinazofuata, ubingwa utakuwa umeshatua Msimbazi.

Mchezo mwingine unaopigwa leo unazitanisha timu mbili ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja kulingana na nafasi zao kwenye msimamo wa ligi. Timu hizo ni Mbao FC ambao wapo nafasi ya 14 wakiwa na pointi 24 na Ndanda FC wenye pointi 23 wakiwa nafasi ya 15, wanaokutana kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s