Ifahamu vizuri USM Alger ya Algeria ambayo imeipa kichapo Yanga cha bao 4-0

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga wameanza vibaya hatua ya makundi baada ya kufungwa mabao 4-0 na USM Algers jana Jumapili ya tarehe 6/05.

derby-mca-usma-tiffo-4

Historia ya USM Alger (kwa ufupi)

Timu hii ilianzishwa mwaka 1937 tarehe 5 Julai miaka kadhaa baada ya mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Yanga kuanzishwa.

Inashiriki ligi kuu nchini Algeria wakitumia uwanja wao uitwao Oman Hamad Stadium uliopo jijini Algeries wenye uwezo wa kubeba watazamaji 17500 zaidi ya watu 42,500 ya uwanja wa taifa la Tanzania, wanavaa jezi nyekundu nyumbani na nyeupe ugenini.

Timu hii ina asilimia kubwa ya wachezaji wazawa kutoka Algeria isipokuwa mmoja tu, imeelezwa. USM Alger ni bingwa wa ligi ya Algeria mwaka 2015.

Licha ya hapo wameshachukua mara 6 huko awali, mafanikio yao makubwa kimataifa ni kucheza fainali ya ligi ya mabingwa afrika dhidi ya Tp Mazembe mwaka 2015/2016.

USM Alger ni miongoni mwa timu 19 bora kwenye rank za timu za Afrika, ya kwanza Algeria, ya 327 kwa dunia kiujumla. Wameingia hatua ya makundi baada ya kuitoa Plateu United ya Nigeria kwa kuichalaza goli 4-0 nchini Algeria mchezo wa marejeano USM Alger walifungwa goli 2-1.

Katika kundi la Yanga, kundi D, hii ndio timu kubwa na kuonekana bora zaidi kulinganisha na nyengine, Oussama Dafalou ndiye mshambuliaji wao kinara anayeongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi ya Algeria amefunga goli 16 katika ligi.

Kwa sasa USM Alger inashika nafasi ya 6 katika ligi, sifa yao kubwa ndiyo timu inayoongoza kwa mashabiki wake kutokaa katika viti, wao husimama na kushangilia mtindo wa namna yake unaitwa Tifo.

Kichapo cha 4-0 kwa Yanga (6/05/2018)

Usiku wa tarehe 6/05 kuamkia leo tarehe 7/05 huko jijini Algiers, Yanga, wamepoteza mchezo wao wa  kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ugenini dhidi ya U.S.M Alger kwa kuchezea kichapo cha mabao 4-0 na kushika mkia katika kundi D.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Julai 5, wenyeji walionekana kutawala na kutengeneza nafasi nyingi za mabao tofauti na Yanga ambao walionekana kucheza kwa kujilinda zaidi.

Yanga iliruhusu mabao mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongezwa mengine mawili kipindi cha pili na kufanya waondoke bila alama huku wakiwa na deni kubwa la mabao ya kufungwa.

Aidha, katika Kundi D, Yanga inashika nafasi ya nne ambayo ni ya mwisho baada ya mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa usiku huo huo kati ya wenyeji Rayon Sport ambao walitoka sare ya bao 1-1 na Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Hata hivyo, kundi D sasa linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye alama 1 sawa na Rayon Sports yenye alama moja pia huku Yanga ikiwa haina alama baada ya kupoteza mechi yake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s