El Clasico yakosa mbabe, zararuana mabao 2-2

Vinara wa La Liga, Barcelona, wameendelea kuifukuzia rekodi ya kumaliza msimu bila kupoteza mchezo katika ligi hiyo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Real Madrid, mtanange uliochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Camp Nou.

messironaldo2012a

Mchezo huo ulioteka hisia za mashabiki wengi wa soka, ulianza kwa kasi na katika dakika ya 10 ya mchezo, straika Luis Suarez alitikisa wavu wa Madrid kwa kuiunganisha krosi tamu ya Sergi Roberto.

Real Madrid haikuonesha kukata tamaa na hilo lilidhihirika dakika nne tu baada ya Suarez kufungua akaunti ya mabao, kwa supastaa Cristiano Ronaldo kuisawazishia timu yake ya Madrid, akiumalizia mpira uliopigwa kwa kichwa na Karim Benzema.

Ronaldo alifunga bao hilo katika mazingira magumu, kwani wakati anaumalizia mpira uliopigwa na Benzema, alijikuta akiumizwa mguuni na beki wa Barca, Gerard Pique ambaye alikuwa akijaribu kuokoa hatari langoni mwake na kuzua hofu kwa mashabiki wa Madrid kutokana na kuchechemea kwa staa wao huyo.

Hata hivyo, madaktari wa Madrid walijitahidi kumtibu Ronaldo na alifanikiwa kurudi dimbani kumalizia dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kukamiana na zilishuhudiwa kadi tano za njano zikitolewa kwa nyota wa timu zote mbili, huku Roberto akijikuta akioneshwa kadi nyekundu katika dakika ya 45, kwa kitendo kilichodaiwa kuwa si cha uanamichezo kwa beki wa Madrid, Marcelo.

Barca ilirudi kipindi cha pili vizuri na kupata bao la pili lililopachikwa kiustadi na Lionel Messi, aliyepokea pasi ya Suarez na kuwapiga chenga wachezaji kadhaa wa Madrid kabla ya kuutumbukiza mpira wavuni.

Kwa mara nyingine tena, Madrid walipambana kuhakikisha hawaondoki Camp Nou kwa aibu, ambapo katika dakika ya 72, winga Gareth Bale alifunga bao zuri baada ya kuzawadiwa pasi ya mwisho na Marco Asensio.

Kufuatia matokeo hayo, Barcelona imebakiza mechi tatu tu ili iweze kumaliza msimu huu bila kupoteza mchezo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s