Huku Ronaldo kule Salah, patamu hapo!!

Unaweza kumwambia Cristiano Ronaldo kaa chonjo, saa mbaya, au unaweza kusema kuwa Ronaldo kwa sasa yupo njia panda baada ya ukweli kuwa, uwezekano wa kutwaa Ballon d’Or msimu huu ni mdogo. Yaani amebanwa kinoma.

Ukiachana na Lionel Messi, ambaye wamekuwa wakichuana kwa miaka 10 mfululizo, sasa kuna amechomoza katikati yao na kuwa tishio kwelikweli, anaitwa Mohamed Salah. Staa huyu wa Liverpool anasumbua.

Ronaldo-Salah

Jumanne usiku ya Mei mosi, kikosi cha Real Madrid kilionyesha shoo ya kibabe na kutoka sare ya mabao 2-2 na Bayern Munich na wakawaondoa wakali hao wa Ujerumani kwa jumla ya mabao 4-3. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa jeshi la Zinedine Zidane kutoka Allinz Arena na ushindi wa mabao 2-1.

Ukiachana na mechi hiyo, kesho yake jumatano usiku, Liverpool ilikuwa ikikamuana na AS Roma katika mechi ya nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Liverpool wakiwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-2 waliyopata katika mchezo wa kwanza pale Anfield.

Kama Liverpool yenye Salah ikitua fainali, basi itakutana na Real Madrid yenye Ronaldo, wachezaji hao licha ya kuanzisha shughuli kubwa katika michuano hiyo, pia wanaingia katika hekaheka za kuwania Ballon d’Or.

Wawili hao wameonyesha kiwango cha maana katika michuano yote msimu huu, lakini unaweza kujiuliza nani ni zaidi ya mwenzake?

cristiano-ronaldo-eibar_1vt81fq2bcvkp1duhqhoich5by

Ronaldo alianza kwa kusuasua katika Ligi Kuu Hispania, lakini ‘alifufuka’ baadaye na kuanza kufunga, kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye ligi akiwa na mabao 24 nyuma ya Lionel Messi ambaye ana mabao 32 huku Louis Suarez akiwa katika nafasi ya tatu kwa jumla ya mabao 23.

Wakati msimu ulipofikia nusu, Ronaldo alikuwa na mabao manne na hiyo ilizua minong’ono kwamba, supastaa huyo hakuwa na maisha marefu ya soka, lakini aliibuka upya na sasa ana mabao 43 katika michuano yote, na amecheza jumla ya mechi 43 katika michuano yote msimu huu na anaonekana kutenda haki katika mechi hizo.

Hakuna ubishi kwamba Messi amekuwa na kasi ya mabao zaidi ya Ronaldo msimu huu akiwa amefunga jumla ya mabao 45 katika michuano yote 53 aliyocheza msimu huu, lakini uwezekano wa kuwania tuzo utakuwa mdogo kwani, Barca haina cha kujifunia kabisa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kuchemsha kwa Barca kumemuondoa Messi kwenye vita hiyo na Salah ameingia kundi la wababe hao wa Ballon d’Or.

Salah

Salah amefunga mabao 45 katika michezo 51 aliyocheza msimu huu, na kizuri ni kuwa ameifikisha timu yake nusu fainali ya Ulaya (Jana alikuwa uwanjani kuwania fainali na kama mambo ni poa basi atakuwa anawania ubingwa Mei 26.) hili linamwingiza katika harakati thabiti za kupambana na Ronaldo.

Kiwango cha Salah kimefanya kuwe na tetesi kwamba huenda mchezaji huyo akatua Real Madrid, lakini ni vipi mchezaji huyo raia wa Misri anakimbizana kwa karibu na Ronaldo, ambaye ni mkali wa soka duniani?

Namba zinaongea

Wakati mitandao kadhaa ikisema kwamba, Ronaldo ana uwezo wa kufunga bao kila baada ya dakika 80 huku Salah akionekana kuwa na uwezo wa kufunga bao kila baada ya dakika 90. Taarifa za mtandao wa Opta zinasema, Salah anahitaji wastani wa mashuti 4.41 kabla ya kufunga bao wakati Ronaldo anahitaji wastani wa mashuti 6.35 kabla ya kupata bao.

Ukiachana na hayo, Salah anaongoza kwa kutengeneza krosi za mabao na hadi sasa amesaidia upatikanaji wa mabao 10 wakati Ronaldo amepiga asisti saba. Hapa unaweza kuona jinsi Salah, ambaye amekuwa injini ya Liverpool anataka kumaliza msimu na kitu gani.

Hata hivyo, Messi ndiye mkali katika idara hiyo ambapo, amepiga asisti 16 mpaka sasa. Lakini, mastaa wengine wa Ligi Kuu England, Paul Pogba na Harry Kane wenyewe huenda wakazisikia tuzo hiyo kwenye luninga kutokana na timu zao kuchemsha Ligi ya Mabingwa Ulaya na mashindano mengine.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s