Wembley kupigwa bei!! A-Z sakata la uuzwaji wa Wembley

Chama cha Soka England (FA) wamepokea ofa yenye thamani ya £800m (pauni 800milioni) ili kuuza Uwanja wa Wembley. Jina la Shahid Khan ndio jina linaongelewa sana baada ya kutoa ofa kwa chama cha soka Uingereza ya kutaka kuununua uwanja wa Wembley.

Wembley

Shahid Khan ni nani?

Shahid Khan ni mpakistani, mzaliwa wa familia ya kisomi nchini Pakistan katika mji wa Lahore ambapo mama yake alikuwa ni profesa wa somo la Hisabati nchini mwao na baba yake akiwa mfanyabiashara nchini humo.

Shahid Khan ndiye mmiliki wa Fulham na timu ya NFL ya Jacksonville Jaguars. Khan ametoa ofa ya kiasi cha £800m (pauni 800milioni) kutaka kununua uwanja wa taifa wa Uingereza, Wembley.

Imeelezwa kuwa, hapo mwanzo Khan aliomba awe anaileta timu yake inayocheza “American Football” katika uwanja wa Wembley walau mara moja kila mwezi, lakini sasa inaonekana anataka kuihanisha kabisa NFL ije Wembley.

Inajulikana kuwa dau hilo limetolewa pauni 500milioni kwa ajili ya uwanja na pauni 300milioni kwa FA. Makamu wa rais wa NFL, Mark Waller alisema wameamua kuchagua London kwa sababu ni sehemu muhimu kwa NFL”.

Katika taarifa yake aliongeza kuwa, “Uamuzi wa kununua Uwanja wa Wembley ni ishara ya Uingereza kujitoa kwao katika kusaidia ukuaji wa mchezo huo. Mahusiano haya mapya yanatoa nafasi ya mchezo wa NFL kukua London.”

Suala hilo limejadiliwa katika kikao cha bodi ya FA kilichokutana leo Alhamisi.

Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000, ndiyo uwanja mkubwa zaidi Uingereza ulijengwa kwa gharama ya pauni 757milioni na ulifunguliwa 2007, imeelezwa.

Nini hatma ya timu ya taifa ya Uingereza?

Inafahamika kwamba uwanja wa Wembley ndio uwanja wa timu ya taifa ya nchini Uingereza, na swali hili limekuwa likulizwa sana mitandaoni kwamba nini kitatokea kama Wembley ikinunuliwa.

Japokuwa vipengele vya mkataba wa uuzwaji wa Wembley kati ya FA na Khan haujawekwa wazi, lakini inaonekana kwamba kati ya jambo ambalo halitabadilika ni timu ya taifa ya Uingereza kuutumia Wembley, na Khan akiununua bado Uingereza watabaki Wembley.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s