Chamberlain hatarini kulikosa Kombe la Dunia, Klopp afunguka juu ya hali yake..

Alex Oxlade-Chamberlain ameweka rehani matumaini ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata maumivu makali ya goti, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tovuti rasmi ya klabu ya Liverpool.

Kiungo huyo aliumia dakika ya 20 katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Liverpool ilishinda mabao 5-2 dhidi ya AS Roma ya Itali.

r360984_1296x729_16-9

Kocha Jurgen Klopp amethibitisha mchezaji huyo ameumia vibaya na anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Fainali za Kombe la Dunia zimepangwa kuanza Juni 14 nchini Russia na Oxlade-Chamberlain anaweza kushindwa kuiwakilisha England, imeeleza sehemu fupi ya ripoti hiyo.

Oxlade-Chamberlain ameanguka mara mbili ndani ya dakika 20 kabla ya nafasi yake kujazwa na Georginio Wijnaldum baada ya kuumia goti la mguu wa kulia alipogongana na Aleksandr Kolarov.

Champions League Semi Final First Leg - Liverpool vs AS Roma
Alex Oxlade-Chamberlain akiwa chini baada ya kupata maumivu makali sehemu ya goti.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, alizungukwa na baadhi ya wachezaji wenzake huku akiwa ameshika sehemu ya goti.

Klopp ameingia hofu kama mchezaji huyo anaweza kurejea katika kiwango chake wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s