Rasmi: Arsene Wenger atangaza kustaafu kuifundisha Arsenal

Hatimaye Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametangaza kustaafu kuifundisha Arsenal mwisho wa msimu huu baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 22.

arsene-wenger_1xxe983hfqc9k1ry8rd9hmppy4

Mfaransa huyo ataondoka katika klabu hapo mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa.

Gunners kwa sasa ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu na wanaweza kumaliza nje ya nne kwa msimu wa pili mfululizo, huku tumaini lao la kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa likiwa limebaki iwapo watachukua ubingwa wa Europa Ligi.

Wenger 1

Wenger (68), ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na Kombe la FA mara saba huku akitwaa mataji mawili mara mbili kati ya mwaka 1998 na 2002.

Wenger amesema alikaa na kutafakari kwa kina kuhusiana na hatma yake na klabu hiyo, ambapo aliamua kukaa na uongozi wa juu wa timu hiyo na kuwaeleza kuwa wakati wake sasa umefikia mwisho.

“Baada ya kutafakari kwa kina kufuatia mazungumzo na klabu yangu, umefika wakati sasa nikae pembeni mwisho wa msimu huu, nina furaha sana kwa muda wote niliokaa hapa klabuni”.

Aliongeza, “Nashukuru kupata nafasi ya kuifundisha klabu hii kwa miaka mingi yenye kumbukumbu, nimeiongoza klabu hii kwa kujitoa kwa moyo wangu wote na akili yangu”.

“Kwa wote wanaopenda Arsenal, yapasa kuchukua jukumu la kulinda heshima ya klabu hii” maneno ya Wenger, kwenye taarifa yake rasmi leo Ijumaa.

Mmiliki mkubwa wa Arsenal, Stan Kroenke alisema uamuzi huo wa leo Ijumaa kuwa “ni moja ya siku ngumu kwa wadau wa michezo baada ya miaka yote.”

Aliongeza, “Moja ya sababu kuingia Arsenal tulikuwa tukitaka Arsene kuipa mafanikio klabu hii ndani na nje ya uwanja” .

Ni nani atakayemrithi?

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel tayari amehusishwa na kazi yake huku Wenger akisema kuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal, Patrick Viera ana uwezo wa kumrithi.

Tuchel anapigiwa debe na wachanganuzi kwa sasa mbele ya kocha wa Ujerumani, Joachim Low na kocha wa zamani wa Real Madrid, AC Milan na Chelsea, Carlo Ancelotti.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s