List ya wachezaji wanaotajwa kuwa wataondoka Man United mwisho wa msimu

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, aliwahi kusema yupo katika mikakati ya kuuza wachezaji nane alionao kwenye kikosi chake. Sanjari na kuuza, Mourinho atatumia fedha itakayouza wachezaji hao kununua wengine ambao watakaokuwa mbadala ili kuimarisha kikosi chake.

maxresdefault

Kwa mujibu wa tovuti ya michezo ya mpira wa miguu, Squawka.com ya nchini Uingereza, imenyetisha listi ya wachezaji 5 wa Man United ambao wanatazamiwa kuwa wataondoka mwisho wa msimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nafasi ya kucheza.

List hiyo ni kama ifuatavyo..

01: Anthony Martial

Martial ametajwa kuwa ataondoka Man United baada ya kugoma kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kutokana na kocha Jose Mourinho kutomchezesha mara kwa mara, hivyo vilabu vya Juventus na Inter Milan vimekuwa vikihusishwa nae kwa karibu, Martial ameanza katika game 16 tu za Man United msimu huu na nafasi yake amekuwa akipewa Rashford.

02: Paul Pogba

Pogba pamoja ya kuwa amenunuliwa kwa pesa nyingi kutoka Juventus na kujiunga na Man United na amefanikiwa kutoa assist nyingi zaidi ya mchezaji yoyote wa Man United katika EPL lakini amekuwa anafanya vizuri kiasi chini ya Jose Mourinho na kuna wakati watu walihoji namna ya Mourinho anavyomtumia kiungo huyo.

03: Marouane Fellaini

Fellaini alikuwa moja kati ya wachezaji wanaopendwa sana na Jose Mourinho msimu uliyoisha lakini maisha yake Man United yanadaiwa kama kukaribia mwisho baada ya kufanikiwa kucheza katika game 19 pekee za mashindano yote msimu huu huku akianza katika game tano pekee na amecheza kwa jumla ya dakika 694.

04: Ander Herrera

Baada ya ujio wa Nemanja Matic ndani ya Man United Herrera ameonekana kuanza kukosa nafasi ya kucheza na amepata kuanza katika game 10 za Man United, hivyo uwepo wa wachezaji wanatajwa kumzidi uwezo kunaweza kumfanya akakimbia Man United na kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza.

05: Luke Shaw

Shaw anatajwa kuwa yeye mwenyewe ameanza kuhisi kuwa hana nafasi tena ndani ya kikosi cha Man United kutokana na nafasi yake kuwa kuna kiungo kama Ashley Young wameanza kucheza hiyo inatokana na jeraha lake la muda mrefu alilolipata msimu uliyopita hivyo anakosa nafasi pia kutokana na kukosa fitness.

Hata hivo, Gazeti la The Daily Express, limeeleza kuwa wachezaji ambao anawapigia upatu Mourinho ni Marco Verratti (PSG), Toni Kroos (Real Madrid FC), Toby Alderweireld (Tottenham Hotspurs) na Samuel Umtiti (FC. Barcelona).

United mpaka sasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imejikusanyia pointi 74 chini ya Manchester City yenye 87.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s