#Road2WorldCup: Fahamu orodha ya Makocha 10 wanaovuta mtonyo mrefu timu za Taifa

Kiu ya mashabiki wa soka ulimwenguni kote inasubiri kushuhudia fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Urusi, mwaka huu.

Jumla ya mataifa 32 kutoka sehemu mbalimbali duniani yatakuwa yakionyeshana kazi katika ardhi ya Urusi, ambao wameweka historia ya kuandaa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

1

Miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuwa na presha kubwa ni makocha wa timu shiriki ambao watakuwa na kibarua kizito kwa kuhakikisha wanatwaa taji hilo ambalo hivi sasa linashikiliwa na Ujerumani.

Ifuatayo ni orodha ya makocha 10 wanaovuna mkwanja mrefu ambao wanatarajiwa kutupiwa macho nchini Urusi.

01: Joachim Low – Ujerumani

01

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani, ambaye ndiye anashikilia taji hilo alilolitwaa nchini Brazil kwa kuifunga Argentina bao 1-0.

Huyu ndiye kinara katika orodha ya makocha wanaoingiza mkwanja mrefu akijikusanyia kiasi cha Euro milioni 3.85 ambazo ni sawa na Sh bilioni 10.8 za Kitanzania kwa mwaka.

02: Adenor Bacchi (Tite) – Brazil

Tite

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Brazil, anashika nafasi ya pili katika orodha ya makocha wanaovuna mkwanja mrefu kwa makocha watakaoonyeshana kazi Urusi kuanzia Juni 14.

Mkufunzi huyo anachukuwa kiasi cha Euro milioni 3.50 ambazo ni sawa na Sh bilioni 9.8 za Kitanzania kwa mwaka.

03: Didier Deschamps – Ufaransa

03

Nyota wa zamani wa Ufaransa ambaye alistaafu kucheza soka mwaka 2001, amepewa dhamana ya kuliongoza Taifa hilo nchini Urusi, hizi zikiwa fainali za pili mfululizo kukiongoza kikosi hicho.

Anashika nafasi ya tatu katika orodha ya makocha wanaovuna mkwanja wa Euro milioni 3.5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 9.7 za Kitanzania, atakuwa na kibarua kizito nchini Urusi kuthibitisha ubora wake.

04: Julen Lopetegui – Hispania

lopetegui

Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania, ambaye amekabidhiwa kijiti cha kuwaongoza ‘La Furia Roja’, anashika nafasi ya nne katika orodha ya makocha wanaovuta mkwanja mrefu akiweka kapuni kiasi cha Euro milioni 3 sawa na Sh bilioni 8.4 za Kitanzania.

05: Stanislav Cherchesov – Urusi

008

Huyu ni mlinda mlango wa zamani wa Umoja wa Kisovieti pamoja na Taifa la Urusi, pia alikuwemo kwenye kikosi cha taifa hili kilichoshiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 na 2002.

Cherchesov, alipewa kibarua cha kuinoa Urusi mwaka 2016 na aliingoza timu hiyo katika mashindano ya kombe la mabara, kwa sasa pia amepewa dhamana ya kukiongoza kikosi cha waandaaji wa fainali hizo. Kabla ya kupewa kibarua cha timu ya taifa, kocha huyu amewahi kuzifundisha klabu za Dynamo Moscow na Legia Warsaw.

Anashika nafasi ya tano katika orodha ya makocha wanaovuna mkwanja mrefu akivuna kiasi cha Euro milioni 2.6 ambazo ni sawa na Sh bilioni 7.3 kwa mwaka.

06: Fernando Santos – Ureno

09

Beki kisiki wa zamani wa Ureno, ambaye amecheza jumla ya michezo 161 akiwa na jezi ya Taifa hilo, alianza kazi ya ukocha mwaka 2010 amekabidhiwa bendera kuhakikisha anarudi na taji nyumbani.

Kocha huyo anakunja kiasi cha Euro milioni 2.25 ambazo ni sawa na Sh bilioni 6.3 za Kitanzania kwa mwaka mmoja.

07: Carlos Queiroz – Irani

07

Kocha mkuu wa kikosi cha Irani, ambaye pia aliwahi kufanya kazi na mkongwe, Sir Alex Ferguson, katika kikosi cha Manchester United, anashika nafasi ya saba katika orodha ya makocha wanaovuna mkwanja mrefu akichukuwa kiasi cha Euro milioni 2 sawa na Sh bilioni 5.6 za Kitanzania kwa mwaka.

08: Gareth Southgate – England

05

Kiungo wa zamani wa England, ambaye amepewa dhamana ya kuwaongoza ‘Three Lion’ katika ardhi ya Urusi anashika nafasi ya nane katika orodha ya makocha wanaovuna mkwanja mrefu akichukua kiasi cha Euro milioni 2 sawa na Sh bilioni 5.6 za Kitanzania kwa mwaka.

09: Jorge Sampaoli – Argentina

04

Kocha wa zamani wa Chile na klabu ya Sevilla, amekuwa akisifika kwa kufundisha soka lake la kushambulia hivi sasa anaiongoza timu ya Taifa ya Argentina ambayo mwezi uliopita ilikumbana na kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Hispania.

Mkali huyo anavuna kiasi cha Euro milioni 1.8 ambazo ni sawa na Sh bilioni 5 za Kitanzania kwa mwaka.

10: Oscar Tabarez – Uruguay

10

Beki wa zamani wa Uruguay ambalo ndilo Taifa la kwanza kutwaa taji la Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, hii inakuwa mara ya tatu mfululizo kuiongoza timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa kuanzia mwaka 2010.

Ndiye anafunga orodha ya makocha wanaovuta mkwanja mrefu ambao wanatarajia kuonyeshana umwamba nchini Urusi, akijikusanyia kiasi cha Euro milioni 1.7 ambazo ni sawa na Sh bilioni 4.8 za Kitanzania kwa mwaka.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s