Man United: Willian ndani, Mata nje Old Trafford

Manchester United wanataka kumsajili Willian kutoka Chelsea na kufungua milango ya Juan Mata kuondoka Old Trafford, imeelezwa.

maxresdefault

Hata hivyo, ripoti iliyotolewa na gazeti la The Sun, ilidai kuwa, Kocha Jose Mourinho anataka kumsajili nyota huyo wa Chelsea, Willian mwisho wa msimu huu na kuziba nafasi ya mchezaji huyo anayetaka kuondoka.

Mbrazil (29), bado ameonyesha anataka kubaki Chelsea, lakini Man United wanaamini wanaweza kukamilisha uhamisho huo sasa.

Mkataba wa Willian ndani ya Stamford Bridge utamalizika 2020 na wanataka pauni 30milioni kiasi ambacho walitumia kumnunua nyota huyo kutoka Shakhtar Donetsk miaka mitano iliyopita.

Mourinho anataka kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kwa lengo la kuweza kushinda na Manchester City msimu ujao.

Mata (30) aliyesajiliwa kwa uhamisho uliovunja rekodi wa pauni 37.1milioni mwaka 2014 amefanikiwa kucheza mechi 182, na kufunga mabao 39. Lakini ameshindwa kuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Mourinho.

Mkataba wa Mata ndani ya Old Trafford utamalizika 2019, baada ya kuwepo katika mkataba huo cha kuongeza mwaka mmoja.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s