Umeisikia hii ya Salah kutua Old Trafford? inshu nzima hii hapa..

Ndiyo hivyo bana, Manchester United imeamua kuanzisha ugomvi wa makusudi na wapinzani wao wa jadi Liverpool kabla ya dirisha la usajili wa majira ya kiangazi halijafunguliwa.

salah

Ishu yenyewe ipo hivi, wababe hao wa Old Trafford wameripotiwa kumtazama supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah ndiye mchezaji anayefaa kabisa kwenda kucheza kwenye timu yao msimu ujao na hivyo wanamfungia kazi ili kupata huduma yake mwishoni mwa msimu huu, imeelezwa.

Salah ametua Liverpool mwaka jana tu, lakini staa huyo wa kimataifa wa Misri ameonyesha kiwango bora kabisa huko Anfield na kufunga mabao kibao kwa msimu huu. Salah amefunga zaidi ya mabao 37 katika mechi 42 alizocheza msimu huu katika michuano tofauti akiwa na jezi za Liverpool.

Liverpool imeshaweka wazi haiwezi kusikiliza ofa yoyote ile kuhusu mchezaji wake huyo, lakini hilo haliifanyi Man United kushindwa kabisa kurusha ndoano yao.

Kwa mujibu wa mtandao wa redio ya michezo Uingereza, talksport, imedai kuwa, ripoti zandani zinadai Man United imepanga kupeleka ofa ya Pauni 175 milioni kama dau lake la kuanzia katika kuinasa huduma ya Salah na kwa mkwanja huo inaamini, Liverpool italegeza kamba na kukubali kufanya biashara.

Real Madrid nayo imekuwa ikihusishwa na mpango wa kuitaka huduma ya staa huyo wa zamani wa Chelsea licha ya ripoti za karibuni kuelezwa imebwaga manyanga kumfukuzia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s