Huyu ndio N’Zonzi, mambo 10 usiyoyajua kuhusu nyota huyu

Hivi majuzi ziliibuka tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba Arsenal wamekubali kutoa pauni milioni 35 kuinasa huduma ya kiungo mshambuliaji wa Sevilla, Steven N’Zonzi.

Nzonzi

Mtandao wa El Gol Digital ulinyetisha kuwa, nyota huyo atatimka Hispania na kuelekea Kaskazini mwa Jiji la London pindi tu dirisha la usajili litakapo funguliwa.

Hata hivyo, huenda mashabiki wa Ligi Kuu England wangependa kuyajua mambo haya kuhusu Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29.

01: Wazazi wake ni raia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mwaka 2011 aliitwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya Taifa, lakini alikataa na kuamua kuiwakilisha Ufaransa.

02: Akiwa kwenye ‘academy’ ya PSG, alitakiwa kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati kutokana na urefu wake, lakini baadaye alihamia kwenye kiungo mshambuliaji, nafasi ambayo anaicheza hadi sasa.

03: Hata kabla ya umaarufu wake, mashabiki wa soka nchini Ufaransa walikuwa wanamtaja kuwa ndiye atakayevivaa viatu vya mkongwe Patrick Vieira katika kikosi cha timu hiyo ya Taifa.

04: Aliyemtambulisha Ligi Kuu England ni kocha mwenye heshima kubwa nchini humo, Sam Allardyce, ambaye alimsajili mwaka 2009 katika kikosi chake cha Blackburn Rovers.

05: N’Zonzi ana historia nzuri na Arsenal, kwani bao lake la kwanza akiwa England alilifunga katika mchezo dhidi ya timu hiyo. Hata hivyo, mtanange huo ulimalizika kwa Arsenal kushinda mabao 6–2.

06: Arsenal watakumbuka pia kadi nyekundu ya kwanza kwa Nzonzi akiwa England aliipata dhidi yao. N’Zonzi alilimwa ‘red’ kwa kumchezea rafu mbaya Laurent Koscielny na nyota huyo alifungiwa mechi nne.

07: Alipotua Stoke City mwaka 2012, mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Manchester City na alitajwa kuwa nyota wa mchezo. Ni mtanange ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao lake la kwanza akiwa na uzi wa timu hiyo aliwafunga Tottenham.

08: Achana na mastaa waliojaa La Liga, N’Zonzi ndiye Mchezaji Bora wa Januari, mwaka huu. Itakumbukwa kuwa, Malaga walimng’oa Stoke kwa ada ya Pauni milioni 7.

09: N’Zonzi alikaribia kuiwakilisha timu ya Taifa ya England katika michuano ya kimataifa. Hata hivyo, wakati baba yake anawasiliana na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho mwaka jana, tayari N’Zonzi alikuwa ameshaichezea U-21 ya Ufaransa.

10: Nje ya uwanja, Nzonzi ni miongoni mwa wanasoka watukutu. Ni kama ilivyotokea mwaka 2013 alipo korofishana na mwendesha baiskeli mmoja nchini England. Lakini pia, mwaka 2015 alimtandika mkewe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s