Huyu ndio Lionel Messi, na marafiki wake wa 5 wa karibu

Tukisema rafiki wa kufa na kuzikana wa Lionel Messi, bila shaka atakuwa mke wake kipenzi, Antonella Roccuzzo. Leo tunaangazia marafiki 5 wa karibu wa nyota huyu mahiri wa vinara wa ligi ya Hispania, Fc Barcelona ambaye anatajwa kuwa mchezaji wa kipekee duniani hasa kwa kuangalia namna ya uchezaji wake dimbani pamoja na mafanikio aliyoyapata katika soka.

messi

Bila shaka kila binadamu ana marafiki, hata Messi naye ana marafiki. Anyway, tuangazie marafiki wa 5 wa karibu wa Lionel Messi “La Pulga” ambaye tayari amejihakikishia namba katika kikosi cha Argentina, katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Russia baadaye mwaka huu.

(kwa msaada wa mtandao wa Sokkaa.com, Kigali, Rwanda)

5. Sergio Aguero- Manchester City

Aguero ni mshambuliaji wa klabu ya Manchester City ambaye pia ni raia wa Argentina. Wawili hawa wanatajwa kuwa marafiki wa karibu sana licha ya kuwa hawachezi klabu moja.

Messi na Arguero walikuwa miongoni mwa wachezaji waliopata medali za dhahabu kwenye mashindano ya Olympic mwaka 2008 wakiwa na timu ya taifa ya Argentina. Wanatajwa kuwa marafki tangu walipokuwa wadogo.

4. Luis Suarez- Barcelona

Suarez ni mchezaji wa klabu ya FC Barcelona ambako anacheza Messi. Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uruguay.

Messi na Suarez ni marafiki wa karibu tangu Suarez alipojiunga na FC Barcelona akitokea katika klabu ya Liverpool nchini Uingereza. Mara nyingi Messi na Suarez huwa pamoja nje na hata ndani ya dimba. Kwa kifupi hutumia muda mwingi kuwa pamoja.

3. Neymar- PSG

Neymar ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya PSG ya Ufaransa. Messi na Neymar wamekuwa marafiki tangu Mbrazili huyo ajiunge na Fc Barcelona.

Neymar alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliowahi kuunda safu ya hatari ya ushambuliaji iliyojulikana kwa jina maarufu la MSN (Messi, Suarez, Neymar).

MSN ilikufa baada ya Neymar kujiunga na PSG kwa ada ya pauni milioni 198 mwishoni mwa msimu uliopita. Licha ya Neymar kujiunga na PSG bado urafiki wa Messi na Neymar huko palepale.

2. Cesc Fabregas- Chelsea

Fabregas ni raia wa Hispania. Huyu ni mchezaji wa klabu ya Chelsea ya Uingereza pia amewahi kuchezea katika klabu ya Arsenal na Barcelona.

Messi na Fabregas ni marafiki wa karibu sana tangu walipokuwa wakicheza katika akademi ya Barcelona ijulikanayo kwa jina la La Masia. Mke wa Messi na mke wa Fabregas pia ni marafiki, na urafiki wao unatokana na urafiki uliokomaa kati ya Messi na Fabregas, imeelezwa.

Mwaka 2015 Fabregas alipoulizwa anaonaje kama Chelsea itamsajili Lionel Messi ili wacheze pamoja, Fabregas alijibu kwa kusema ni kitu ambacho anakiota siku moja kitokee na atafurahi sana kama itatokea.

Mara kadhaa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja katika jiji la London.

1. Dani Alves- PSG/Barcelona

Dani Alves ni raia wa Brazil, pia mchezaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa kwa sasa, lakini amewahi kucheza na Messi katika klabu ya Barcelona kabla ya kutimkia Italia kwenye klabu ya Juventus.

Messi anasema urafiki wake na Dan Alves ni wa kipekee tangu wawili hao walipokuwa wakicheza pamoja dimbani na kutengeneza muunganiko mzuri kati yao japokuwa Alves yeye anakipiga katika nafasi ya ulinzi wa kulia.

Messi anasema Dan amekuwa rafiki yake kwa muda mrefu, wamekuwa pamoja kama marafiki kwa miaka mingi, na hiyo ilisaidia kuelewana vizuri walipokuwa dimbani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s