#Road2WorldCup: Fahamu juu habari hizi 6

Maisha yanakwenda kasi sana, zimebaki siku chache tu kabla ya kupigwa kwa mtanange wa Kombe la Dunia kule Russia 2018. Mwaka huu kila nchi inataka ubingwa ili kutanua historia yake.

Lakini, katika fainali hizo kuna timu 32 zitawania nafasi ya kutwaa taji hilo, ambalo ni  timu nane tu ambazo zimewahi kufanikiwa kulitwaa. Hapa nime kuwekea ‘SIX BIG STORIES’ ambazo huenda zilikupita kuelekea mashindano hayo.

06: Neymar amtabiria makubwa Salah

468017314.0

Supastaa wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar amemtabiria makubwa staa wa Misri, Mohamed Salah, kuwa atafanya makubwa kule Russia.

Neymar anaamini Salah atakuwa na kiwango bora na kuwa moja ya wachezaji watakaotamba kwenye fainali hizo. Akizungumza kwenye mahojiano na mtandao wa FourFourTwo, Neymar alidai..

“Salah ni mchezaji mzuri na ataonyesha utofauti mkubwa kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Watu wasubiri kumuona.”

Mbali na Salah, Neymar ameitaja timu ya taifa ya Ubelgiji kuwa, itafanya vizuri na kuwashangaza wengi.

05: Weah akiri kuikubali timu ya Taifa ya Nigeria kinoma!

george-1024x576

Gwiji wa soka wa zamani wa Liberia na Rais wa nchi hiyo George Weah, ameitabiria timu ya taifa ya Nigeria kufanya vizuri kwenye michuano hiyo inayoanza kutimua vumbi Juni 14.

Weah alitoa utabiri wake wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari nyumbani kwake jijini Lagos, akiwa kwenye ziara ya kikazi nchini humo hivi karibuni.

Alisema kikosi cha Nigeria kilichofuzu fainali za mwaka huu kama timu ya kuigwa na mataifa mengine ya Afrika yaliyofuzu fainali hizo kutokana na ubora wake, iliandika tovuti ya Premium Times, Nigeria.

Pia, aliwashauri kujiandaa mapema ili waweze kufika mbali kwenye fainali hizo.

“Nigeria wanakwenda kuwakilisha Afrika na nitakuwepo kuwatazama. Kwa kikosi walichonacho kina uwezo wa kufika mbali ikiwezekana na kutwaa ubingwa,” alisema Rais Weah.

04: Waamuzi England wapigwa ‘Stop’

1478884871_433087_1478885086_noticia_normal

Jumla ya Waamuzi 36 tayari wametangazwa kuchezesha mashindano ya michuano ya Kombe la Dunia, nchini Urusi.

Gumzo kubwa orodha hiyo ni kukosekana kwa Waamuzi kutoka taifa la England na sababu inayotajwa ni kushindwa kumudu kuchezesha vizuri.

Inaelezwa kuwa England imekuwa na Marefa ambao wamekuwa wakiboronga kuchezesha na hicho kinawezekana kikawa kigezo kikubwa cha kushindwa kuteuliwa kuhusika kwenye Kombe la Dunia mwaka huu.

Mbali na England, FIFA pia hawajatoa hata Mwamuzi mmoja kutoka Mataifa ya nchi za Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini.

Uamuzi huo wa FIFA umewafanya wadu wa soka kila mmoja kuzungumzia lake baada ya uteuzi huo kufanyika.

03: Mbuzi, mnyama rasmi kutabiri matokeo ya mechi za Kombe la Dunia, 2018

zabiyaka

Baada ya kushuhudia Samaki aina ya Pweza akitabiri matokeo ya mechi za Kombe la Dunia mwaka 2006 kule Ujerumani, huku Ngamia akitumika kutabiri fainali za mwaka 2010 na kobe akitabiri fainali za mwaka 2014, mwaka huu mpango mzima utatolewa kupitia kwa mbuzi kutabiri mechi hizo.

Mbuzi huyo aliyepewa jina la Zabiyaka aliyepo katika mji wa Samara, ambayo ni miongoni mwa miji 11 itakayotumika kwa fainali hizo kule Russia.

Zabiyaka alipata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wanyama wengine kama Mbweha na Tumbiri kwenye kura zilizopigwa za kuchagua mnyama gani atakuwa mtabiri wa mechi za michuano hiyo.

Kinyang’anyiro cha kumpata myama atakayetabiri matokeo ya mechi hizo, kilihusisha viumbe saba kutoka kwenye eneo la kufugia wanyama la mji wa Samara (Samara Zoo).

Viumbe hao ni, Mbuzi (Zabiyaka), Tumbiri (Simon), Ngamia (Lexus), Skunk (Coco), Chatu (Murzik), Mbweha (Richard) na Kuku (Isadora).

02: Pazia la Kombe la Dunia kuchanwa Luzhniki, mjini Moscow

moscow-feb-26-2014-reconstruction-of-soccer-stadium-luzhniki-at-sunny-day-aerial-view_4k9zwem7e__F0000

Fainali za Kombe la Dunia 2018 zitaanza kutimua vumbi Juni 14, kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Russia dhidi ya Saudi Arabia. Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow.

Mbali na mechi ya ufunguzi, uwanja huu pia utatumika katika mechi ya fainali ya michuano hiyo. Luzhniki ni uwanja mkubwa kuliko viwanja vyote vitakavyotumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watu 81,000 walioketi, ukishika nafasi ya kwanza kwa kuchukua idadi ya watazamaji wengi nchini Russia na unashika nafasi ya nane kwenye barani Ulaya, ukizidiwa na viwanja vya Camp Nou (Hispania 99,354), Wembley (England 90,000), Croke Park (Ireland 82,300), Twickenham (England 82,000), Signal Iduna Park (Ujerumani 81,359), Stade de France (Ufaransa 81,338) na Santiago Bernabeu (Hispania 81,044).

Kwa ujumla, Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Russia zitatumia viwanja 12 ambavyo ni: Luzhniki, Otkrytiye, Krestovsky, Kaliningrad, Kazan, Nizhny Novgorod, Cosmos, Volgograd, Mordovia, Rostov, Fisht na Central.

01: Timu ya Taifa ya Russia yapania kufika nusu fainali za Kombe la Dunia, 2018

i

Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, Russia wamepania kufika nusu fainali katika michuano ya mwaka huu.

Ni lengo zuri, kwani Ufaransa ilipoandaa fainali hizo ilitwaa ubingwa jambo ambalo lilikuwa halijafanyika tangu miaka ya 70. Russia imewahi kushiriki katika Fainali 10 tu za Kombe la Dunia, na mwaka huu inashiriki ikiwa mwandaaji wa fainali.

Chini ya kocha mzawa Stanislav Cherchesov, Russia inakwenda katika Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 ikiwa ni mwenyeji.

Katika hatua za makundi ipo kundi A na timu za Saudi Arabia, Misri na Uruguay. Kundi hili Saudi Arabia ndio inaonekana kuwa kibonde, lakini kwa Misri mambo yatakuwa tofauti kwani, wamepania kufika mbali na kuweka historia kwenye michuano hiyo.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s