Salah awakimbiza Cr7, Messi, mbio za kutwaa Kiatu cha Dhahabu Ulaya

Straika wa Liverpool, Mmisri Mohamed Salah, anaongoza mbio za kutwaa Kiatu cha Dhahabu barani Ulaya kufuatia mabao manne aliyotupia dhidi ya Watford wiki moja iliyopita.

KIATU CHA DHAHABU

Tuzo hiyo hutolewa na vyombo vya habari vya Ulaya (ESM), kwa kinara wa ufungaji barani humo, huku nafasi kubwa ikitolewa kwa mfungaji kutoka katika ligi kubwa tano za UEFA, ambazo ni Premier League (England), La Liga (Hispania), Ligue 1 (Ufaransa), Serie A (Italia) na Bundesliga (Ujerumani)

Hapa, katika uchambuzi huu, nimetazamia vinara 10 wanaokimbizana katika mbio za kiatu hicho barani Ulaya… (Kwa msaada wa tovuti ya LiverpoolEcho, Uingereza).

1. Mohamed Salah – Liverpool (mabao 28)

Straika huyu wa kimataifa wa Misri anapewa pointi 56, wakati huu akiwa ameshafumania nyavu mara 28 katika mechi 30 alizocheza na kati ya hizo mechi sita amefunga zaidi ya bao moja ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Watford ambap alitupia manne.

2. Lionel Messi – Barcelona (mabao 25)

Tayari amejikusanyia pointi 50, mshindi huyu wa msimu uliopita anachuana vikali na Salah msimu huu baada ya kutupia mabao 25 kwenye La Liga.

3. Ciro Immobile – Lazio (mabao 24)

Amejikusanyia pointi 48, akiwa amefungana katika nafasi hiyo na wachezaji wengine wawili, lakini nyota huyu wa kimataifa wa Italia yeye amecheza mechi chache zaidi, 26, kuliko Edinson Cavani na Harry Kane wanaolingana wote wakiwa na mabao 24.

Alifunga mabao matatu dhidi ya AC Milan Septemba na manne dhidi ya SPAL Januari, na kupiku mabao yake 23 aliyofunga katika ligi msimu uliopita.

4. Edinson Cavani – PSG (mabao 24)

Straika huyu wa Paris St Germain, tayari anayo mabao 24 na amejikusanyia pointi 48 kwa kazi hiyo aliyoifanya hadi sasa.

Kusajiliwa kwa Neymar na Kylian Mbappe kipindi cha majira ya joto, kungeweza kumuondoa Cavani katika mbio hizi kwani tayari alishaliacha jukumu la kupiga penalti kwa Mbrazil huyo, lakini Cavani kwa mara nyingine tena ameonyesha ubora kwa kucheka na nyavu na anaweza kupiku mabao 35 aliyofunga msimu uliopita kwenye Ligue 1.

5. Harry Kane – Tottenham (mabao 24)

Naye ana pointi 48 baada ya straika huyo wa Spurs na England ambaye ametwaa Kiatu cha Dhahabu Premier League misimu miwili iliyopita, kutupia mabao 24 hadi sasa, lakini majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mechi dhidi ya Bournemouth yakikatisha matumaini yake.

6. Jonas – Benfica (mabao 31)

Kinara huyu wa ufungaji katika orodha hii, anapewa points 46.5, ingawa mabao yake yamepatikana katika Ligi Kuu ya Ureno ambayo haipo kwenye ligi tano bora za Uefa, hivyo hupewa pointi 1.5 tu kwa bao, ukilinganisha na hizo tano kubwa ambazo pointi zinazotolewa ni mbili kwa bao.

7. Robert Lewandowski – Bayern Munich (mabao 23)

Nyota huyu wa kimataifa wa Poland na Bayern, amejikusanyia pointi 46, amekuwa katika mbio hizi katika misimu ya hivi karibuni na hat-trick aliyofunga dhidi ya Hamburg ilimfanya kufikisha mabao 100 kwenye Bundesliga akiwa na klabu hiyo.

8. Cristiano Ronaldo -Real Madrid (mabao 22)

Idadi hiyo inamfanya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno kujikusanyia pointi 44, wakati huu wengi walipokuwa wakihoji kuanza kwake kwa kusuasua mwanzoni mwa msimu pamoja na Real.

Alijibu mapigo baada ya kucheka na nyavu mara nne dhidi ya Girona Jumapili, hivyo kufikisha mabao 14 katika mechi sita za ligi za mwisho alizocheza.

Kwa kipimo kizuri amefunga katika kila mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyocheza msimu huu.

9. Mauro Icardi – Inter Milan (mabao 22)

Ana pointi 44, na kama ilivyo kwa Salah na Ronaldo, Icardi, amefunga mabao manne kwenye mechi moja wiki mbili zilizopita.

10. Sergio Aguero – Man City (mabao 21)

Mabao hayo yanamfanya Muargentina huyo kujikusanyia pointi 42 na kumtoa Luis Suarez wa Barcelona katika 10-bora.

Kadhalika, mabao hayo 21 yamechangia kumfanya kuwa mfungaji bora wa City wa wakati wote na yupo njiani kutimiza mabao 200 katika klabu hiyo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s