Hatimaye Zlatan Ibrahimovic atua Galaxy kwa kishindo

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic tayari amekamilisha uhamisho wake wa kwenda LA Galaxy. Ibrahimovic anayejifananisha na Simba alipost video yake akiwa na jezi ya Galaxy, nakuandika, “Los Angeles, karibu Zlatan.” kupitia ukurusa wake wa Instagram.

Zlatan-Ibrahimovic-LA-Galaxy

Ibrahimovic na Manchester United wameamua kuchana mkataba uliokuwepo baina yao na staa huyo wa kimataifa wa Sweden jana alitazamiwa kuendelea na maisha mengine kwa kujiunga na klabu ya LA Galaxy.

Dili la Zlatan kwenda Galaxy linatazamiwa kuwa mkataba wa pauni 1 milioni kwa mwaka na lilitazamiwa kutangazwa kama tangazo katika ukurasa mzima wa gazeti maarufu la Marekani, Los Angeles Times na alitazamiwa kwenda California kwa ajili ya kutambulishwa, imeelezwa.

20180323-The18-Image-Zlatan-Ibrahimovic-LA-Galaxy-Contract

Zlatan mwenye umri wa miaka 36 amesaini mkataba mpaka mwishoni mwa msimu na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza kwa wababe hao katika pambano la Ligi Kuu ya Marekani dhidi ya watani wao wa jadi LAFC Machi 31.

United ilithibitisha jana kwamba walikuwa wameukomesha mkataba wa staa huyo ambaye kwa mara ya kwanza sasa atacheza nje ya bara la Ulaya baada ya kutamba katika klabu za Barcelona, Ajax, Paris Saint-Germain, Juventus, Inter Milan na AC Milan.

Zlatan mwenyewe aliandika katika ukurasa wake wa Instagram, akisema “Mambo mazuri ufika mwisho na huu ni wakati wa kuendelea na maisha mengine baada ya kuwa na misimu mizuri miwili na Manchester United.”

“Asante sana kwa klabu, mashabiki, timu, kocha na wafanyakazi wengine ambao walishirkiana na mimi katika sehemu hii ya historia yangu.:”

zlatan

Zlatan alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kujiunga na klabu hiyo ambayo iliwahi kuwachukua David Beckham na Steven Gerrard katika nyakati mbalimbali na sasa Zlatan anakwenda kufungua ukurasa mpya klabuni hapo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s