Nyota Real Madrid, Cristiano Ronaldo aanzishiwa zengwe na mrembo huyu..

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameingia kwenye kumi na nane za mrembo wa Kibrazili baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kijinsia, mrembo Erika Canela.

MAIN-Ronaldo-and-Miss-BumBum

Erika Canela, 26, ambaye alishinda katika shindano la Miss Bum Bum Brazil, mwaka 2016, alisema kuwa alipokea ujumbe wa ‘Vitisho na kutukanwa’ baada ya kumbwaga nyota huyo wa Real Madrid wakati alipogundua kwamba alikuwa na mpenzi mwingine.

Licha ya kupasia sana nyavuni na kuibeba klabu yake hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaelezwa kuwa Ronaldo alimtishia pia mrembo huyo kwa kumwambia maisha yake yataharibiwa.

Akiongea na mtandao wa gazeti la The Sun, Canela ametishia kumshitaki mahakamani Ronaldo kwa kumfanya kupitia kwenye kipindi kigumu wakati alipomtema.

“Aliniacha kwenye mazingira magumu na kunipa msongo wa mawazo, pia alinisababishia aibu kubwa kwa watu waliokuwa wakifahamu uhusiano wetu,” alilalamika Canela.

Kwa ufupi, historia ya kimahusiano ya Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo. Si kwamba ni mkali tu wa kutupia mabao uwanjani, bali staa huyu wa Real Madrid, ni balaa kwenye kuchagua warembo.

Tangu mwaka 2002 hadi sasa ameshakuwa kwenye mahusiano na warembo 17. Si mtu wa kutulia na mrembo mmoja kwa muda mrefu.

Na hii ndio sababu iliyofanya mpaka leo watoto wake watatu, Cristiano Jr, Mateo na Eva, kutokujulikana alizaa na mwanamke yupi. Zimebaki kuwa tetesi tu kuwa alipandikiza mbegu.

Baada ya kubwagana na Irina Shanky, hivi sasa yuko kwenye mahusiano na mrembo Georgina Rodriguez, ambaye anaonekana kumtuliza kuliko wanawake wote aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano.

Georgina Rodriguez, 22, mrembo wa Kihispania ambaye tayari ana watoto watatu pamoja na Ronaldo. Moja katika mambo yanayotajwa kumfurahisha Ronaldo ni utulivu wa Georgina ambaye si mrembo anayependa maisha ya kuuza sura kila mara kwenye vyombo vya habari.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s