Rick Ross arejea kwa kishindo jukwaani

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, Rick Ross, amerejea kwa kishindo katika shughuli zake za kawaida baada ya juzi kufanya tamasha kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Light uliopo mjini Las Vegas, Marekani.

rick-ross-performance-2016-a-billboard-1548

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Florida Boy’ aliyoshirikiana na T-Pain na Kodak Black, mapema mwezi huu alidondoka ghafla na kuwahishwa hospitali akidaiwa kuwa na tatizo la nimonia lililompata akiwa nyumbani kwake, Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Hata hivyo hiyo sio mara ya kwanza kuripotiwa kwa taarifa za Rick Ross kupoteza fahamu. Oktoba, 2011 Rozay alianguka mara mbili, huku akidai ni kufanya kazi sana na kukosa usingizi.

Katika tamasha lake, Rick Ross maarufu kama ‘Da Boss’, aliwaeleza mashabiki wake kuwa yupo fiti kuendelea na kazi, imeelezwa.

Baada ya kuimba nyimbo chache Da Boss aliomba polisi wamwachie huru rafiki yake kipenzi Meek Mill ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi la Marekani.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s