Casemiro: Ronaldo na Neymar ni bonge la kombinesheni

Mambo ni moto. Kinachoonekana ni kama vile staa wa Paris Saint-Germain, Neymar anatimkia Real Madrid kama si kwenye dirisha lijalo, basi mapema tu mwakani.

DXor2eTX4AMhVJ0

Unajua kwanini, kiungo wa Real Madrid, Casemiro, ambaye wanacheza pamoja na Neymar huko kwenye kikosi cha Brazil, amefichua kitu kinachofikirisha baada ya kusema staa huyo aliyewahi kuichezea Barcelona atakwenda kutengeneza kombinesheni matata sana na Cristiano Ronaldo wakati atakapotua Santiago Bernabeu.

Taarifa za Neymar kwenye Real Madrid hazikauki kwa sasa jambo linalowafanya hata mabosi wa PSG kutokuwa na uhakika kama staa huyo ataendelea kubaki kwenye kikosi chao baada ya matokeo ya msimu huu kuboronga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya mechi ya PSG na Real Madrid walipokutana Bernabeu, Ronaldo alionekana kushikana na Neymar na kuzungumza kitu na hilo linamfanya Casemiro aamini kutakuwa na urafiki mzuri sana baina ya masupastaa hao wawili watakapokwenda kucheza pamoja kwenye kikosi cha Los Blancos.

“Neymar siku zote amekuwa matata, tangu alipokuwa na umri wa miaka 11, amekuwa akifanya mambo ya maajabu sana uwanjani,” alisema Casemiro, alipofanya mahojiano na mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid.

“Mi sijui kama atakuja Real Madrid, lakini uthibitisho wa hilo utapatikana kwa kumuuliza rais Florentino Perez. Neymar mwenye anafahamu wazi mlango siku zote upo wake kwake kuja Madrid, lakini anaonekana kuwa na furaha huko Paris.

Aliongeza, “Kwa kiwango chake, kama ingekuwa mimi ningemsajili bila ya kushinda. Natumaini atakuja mwaka huu. Atakuja kutengeneza kombinesheni matata kabisa na Cristiano.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s