#Road2WorldCup: Fahamu juu ya mabadiliko haya

Michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 inayofanyika nchini Russia kuanzia June mpaka July ni tofauti sana na michuano ya nyuma. Kanuni na sheria za nchi hii zina utofauti mkubwa ambao umepelekea mabadiliko kadhaa katika masuala ya logistics na usalama.

01

Moja ya mabadiliko makubwa ni kwamba TIKETI pekee haiwezi kukupa fursa ya kuingia uwanjani kuangalia mechi. Kwanini????? Unahitaji kitu kinachoitwa FAN ID – Kitambulisho cha shabiki!

FAN ID ni kitu gani?

02

Hiki ni kitambulisho au nyaraka ambayo ni lazima uwe nayo ili kuweza kupata fursa ya kuhudhuria mechi za World Cup. Ili kuipata unahitaji kununua tiketi, baada ya hapo unaingia kwenye mtandao wa FIFA (www.fifa.com/tickets) na kujaza fomu maalum ambayo itakuwezesha kupata kitambulisho hicho maalum kwa ajili ya World Cup 2018.

FAN ID ni muhimu na lazima kwa kila shabiki, wageni na raia wa Russia kuwa nayo ili kuweza kupata access ya kuingia viwanjani.

04

Faida za FAN ID

1. Viza – Kwa kawaida upatikanaji wa viza ya kuingia nchini Russia 🇷🇺 ni mgumu sana kutokana na sheria za nchi hiyo hasa katika masuala ya usalama, hili kuondoa kasumba hii wakatengeneza mfumo maalum ambayo utaondoa bugudha kwa wageni zaidi ya millioni na nusu ambao wanategemewa kusafiri kwenda Russia wakati wa kombe la dunia.

05

Unapokuwa na FAN ID pekee utaweza kuingia katika mipaka ya nchi hii ya Russia. bila kuhangaika kupata Visa. Hii ni moja ya faida kubwa ya kitambulisho hiki, hivyo unahitaji pasi ya kusafiria, tiketi yako na FAN ID ambayo mamlaka za Russia wanaitumia kama kadi ya kutambua wageni.

2. Kupata fursa ya matumizi ya usafiri wa ndani bure — Unapokuwa na kadi ya shabiki itakuwezesha kupata fursa ya kutumia mabasi na treni maalum kwa ajili ya World Cup bila malipo yoyote, kadi yako itatosha kukupa fursa ya kutumia usafiri huo bila kutumia hata sunni.

Web

Unachohitaji kufanya ili kupata fursa hii kujisajili kupitia mtandao wa tickets.transport2018.com. Humu utahitajika kujaza fomu ambayo itahitaji kujua mji unaotaka kwenda, na kuangalia mechi gani, siku na muda, hivyo watahitaji uweke taarifa za tiketi za mchezo husika unaotaka kwenda kuangalia. Ujanja ujanja hakuna.

Bila kuwa na FAN ID na tiketi inayoonyesha unataka kwenda kuangalia mchezo gani, utakosa nafasi ya kutumia treni maalum kwa ajili ya mashabiki. Usajili wa usafiri wa bure inabidi uufanye masaa 24 kabla ya muda wa safari yako!

img_4411

Kuna Train maalum 500 zitakazokuwa zinasafirisha baina ya mikoa 11 ambayo itatumika kwa ajili ya mechi za Kombe la dunia 2018.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s