Wazazi wa Akwilina waeleza jinsi kifo chake kilivyofuta ndoto zao za kujikomboa na umaskini mkubwa

Kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha taifa cha usafarishaji, NIT, Akwilina Akwilini kimeitikisa nchi. Kuuawa kwa risasi kwa binti huyo kumesababisha huzuni kwa kila mtu. Lakini ni nani mwenye huzuni zaidi kuwazidi wazazi wake?

 

Hakuna. Kwa Mzee Akwilin Shirima wa Rombo mkoani Kilimanjaro, kifo cha mwanae kimeyazima matumaini ya siku moja kuja kujikomboa kwenye hali ya umaskini aliyonayo. Kwa tabu sana, binti yao aliyekuwa na uchungu mkubwa wa kuisaka elimu kwa udi na uvumba hadi kufanikiwa kupata udahili katika chuo cha NIT, alikuwa amepania kubadilisha maisha ya wazazi wake.

Kifo, cha kutisha kilichomkuta katika harakati za kutafuta nafasi ya mafunzo kwa vitendo kimeikatili ndoto yake. Kwenye mahojiano na MCL Digital, Mzee Akwilini amesema tangu apewe taarifa hizo mbaya hali, hanywi. “Serikali iniangalie, sina pa kwenda, sina mbele wala nyuma,” amesema kwenye mahojiano hayo.

Rafiki wa familia hiyo, Dismas Shirima amemwelezea marehemu Akwilina kama binti aliyekuwa na uchu mkubwa na elimu. Amedai kuwa wazazi wake walikuwa hawana uwezo wa kumsomesha na hivyo alisaidiana pamoja na shangazi yake na ufadhili wa watu wengine.

“Nilipomuuliza kwanini yeye alikuwa anapenda kusoma alikuwa anazungumzia kwamba mimi nataka nisome ili nisiwe kwenye hali ya umaskini kama ninavyoona wazazi wangu wapo katika hali ya umaskini, naamini kwamba nikisoma nitaweza kuifanyia kazi, nitaisaidia jamii na vile vile nitaisaidia familia.’

Amesema kutokana na kuwa na uchu huo wa kuisaka elimu watu wengi walipenda kumsaidia. Pia amedai upole wake ulimfanya awe kipenzi cha wengi nyumbani kwako.

Kwa sasa shughuli za mazishi zinaendelea ambapo ndugu wa marehemu waliopo Dar es Salaam wamedai gharama ya mazishi inakadiriwa kuwa shilingi milioni 80 na kwamba licha ya serikali kuahidi kugharamikia, wao wanaendelea kuikusanya kupitia michango ya ndugu na marafiki.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s