Nataka kiungo wa kumrithi Carrick si Pogba – Mourinho

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameweka wazi kuwa lengo lake la kumsajili kiungo mwingine mwisho wa msimu ni kuziba nafasi ya Michael Carrick siyo Paul Pogba.

maxresdefault

Mourinho alitumia muda mwingi wa mkutano wake na wanahabari kuelekea mchezo wa Kombe la FA dhid ya Huddersfield Town kujibu maswali juu ya hatma ya Pogba baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa wawili hao kwa sasa hawana maelewano mazuri.

Gazeti la Ufaransa la L’Equipe limedai kuwa, Pogba ambaye alijiunga Man United akitokea Juventus kwa uhamisho uliovunja rekodi wa pauni 89.3milioni Agosti 2016, kuwa hana furaha ya kuchezeshwa kiungo mkabaji na kudai kwa sasa nafikiria kuondoka Old Trafford.

Pogba ameshindwa kuonyesha kiwango chake katika wiki za karibuni na Mourinho alimtoa kiungo huyo katika mechi mbili kati ya tatu zilizopita za Man United.

Hata hivyo, Mourinho alijibu kwa kusema ni ‘uogo’ kuhusu kiungo huyo Mfaransa kabla ya kusisitiza kuhusu kumalisha safu ya kiungo wa kuziba nafasi ya Carrick, 36, aliyepanga kustaafu mwisho wa msimu huu na kuchukua jukumu la ukocha.

“Tunahitaji kumsajili kiungo mpya,” alisema Mourinho. “Kwa sababu si muda mrefu Michael Carrick ataondoka. Ni wazi tunatakiwa kuweka usawa katika timu.

“Baadhi yenu (vyombo vya habari) wamekuwa wakisema tutamsajili mshambuliaji, wengi winga, winga wa kushoto, winga wa kulia.”

Mreno huyo aliongeza kuwa, “Unaweza kunilaumu mimi kwa mambo mengi, lakini siwezi kusema uogo kwenu. Wakati ninapoamua kunyamaza, siyo kuwa siwezi kuzungumza nayi ili mbadilishe uelekeo.

“Tunaangalia na kutafuta kiungo kwa lengo la kumsajili mwisho wa msimu.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s