Lukaku aahidi kutimkia Anderlecht, baada ya maisha Man United

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku ameahidi atarudi tena kuichezea Anderlecht mara tu maisha yake ya Manchester United yatakapofika ukingoni, imeelezwa.

LUKAKU

Fowadi huyo aliyenaswa na Man United kwa ada ya Pauni 75 milioni mwaka jana, ameshafunga mabao 19 katika kikosi hicho ambacho maisha yake yamekuwa ya kupanda na kushuka.

Lukaku ametengeneza jina lake kuwa kubwa huko England kutokana na mabao yake aliyokuwa akifunga Everton, lakini soka lake la kulipwa alianzia kulicheza huko Ubelgiji kwenye klabu ya Anderlecht, ambako mechi yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 kabla ya kunaswa na Chelsea wakati akiwa na umri wa miaka 18.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka HLN nchini Ubelgiji, Lukaku alisema.“Ndoto zangu siku zote ni kuichezea Anderlecht,”. Aliongeza, “Kabla sijaachana na maisha ya soka kama mchezaji, nitarudi kuichezea timu hiyo, naweza kutoa ahadi hiyo. Nilikuwa na nyakati nzuri sana kule.”

Lukaku anaamini Man United bado wapo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kocha wao, Jose Mourinho kusisitiza mambo yamewashinda.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s