Xavi atabiri mrithi wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi

Kiungo wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Xavi Hernández, anaamini Neymar na Kylian Mbappe ndiyo wachezaji watakaokuja kutamba wakati zama za Lionel Messi na Cristiano Ronaldo zitakapokwisha kwenye kupokezana tuzo ya ubora wa mchezo wa soka duniani, Gazeti la Uingereza la Daily Mail limeripoti.

neymar-mbappe-psg-graphic

Ronaldo na Messi wametawala dunia ya mchezo huo kwa miaka 10 sasa huku kila mmoja akishinda tuzo ya Ballon d’Or mara tano, imeelezwa.

Neymar, kwa upande wake aliikaribia tuzo hiyo msimu uliopita alipokuwa Barcelona na kwamba msimu huu akiwa PSG amepandisha zaidi kiwango chake cha soka na kuwa staa mkubwa kwenye timu hiyo.

Mbappe pia ameibukia vizuri kabisa kutoka Monaco na sasa yupo na Neymar huko PSG.

“Namheshimu sana,” alisema Xavi akimzungumzia Neymar. “Ni mchezaji mahiri, wakati Messi na Cristiano watakapo poromoka viwango vyao, atashinda yeye tuzo inayofuata.

“Kipindi ambacho Messi na Cristiano Ronaldo watastaafu, mjadala wa mchezaji gani bora duniani utakuwa kati ya Neymar na Mbappe.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s