Jux: Vanessa alitamani ahame nchi baada ya kuwekwa rumande mwaka jana

Vanessa Mdee hatousahau mwaka 2017. Alikuwa mmoja wa mastaa waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa wanashukiwa kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya.

Shutuma hizo zilipelekea akae rumande kwa takriban wiki moja. Mpenzi wake, Jux amedai kuwa hicho kilikuwa ni kipindi kigumu zaidi katika maisha ya Vee Money kiasi ambacho alitamani ahame nchi. “Ulikuwa ni muda mgumu sana, alibadilika kabisa, baada ya kutoka kule hakuwa Vanessa yule ninayemfahamu,” Jux alisema kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Kiss FM cha nchini Kenya siku kadhaa zilizopita.

“Alisema ‘nataka kuondoka kwenye nchi hii, yote haya ni sababu ya muziki nisingekuwa Vanessa Mdee isingetokea hii.”

Jux amesema jambo hilo limemfundisha mengi pia Vanessa Mdee.

26870688_1563386950419520_3025900383831588864_n

Kwa upande mwingine Jux amedai kuwa katika muda wote ambao Vanessa alikuwa rumande, alikuwa akishinda hapo hapo kuanzoa asubuhi hadi asubuhi inayofuata.

Hata hivyo Jux amedai kuwa tukio hilo liliongeza chumvi kwenye kidonda katika uhusiano wao kutokana na maneno aliyokuwa akiambiwa Vanessa na watu mbalimbali.

“Iliharibu sana,” alisema Jux. “Unajua kabla ya Vanessa nilikuwa na msichana anaitwa Jacque, alikuwa na matatizo naye alikamatagwa na  mambo fulani hivi ambayo sio poa lakini sikuwa najua kitu. So Vanessa alivyosikia vile akasema ‘Jux labda ni sababu yako sababu bila wewe mimi nisingeitwa hapa.’ So alipotoka akabadilika. Alikuwa na vitu vingi, mtu yeyote akija kwake anamuambia kitu tofauti. Kutoka hapo alipotoka pale ndio tume-break up, tumekuja kupatana hii September I think.”

Jux alimsindikiza Vanessa nchini Kenya kwenda kufanya uzinduzi wa album ya Money Mondays.

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s