Ripoti: Neymar aongoza kuvuna mamilioni Twitter, Instagram

Kweli mwenye nacho huongezewa. Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Neymar, ambaye pia ni mshambuliaji ghali zaidi kwa sasa, anaingiza karibu nusu milioni kwa kila ujumbe wake anaotuma kwenye mitandao yake ya kijamii, imeelezwa.

neymar

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Radio Marca ya nchini Hispania zinasema kuwa utafiti mpya umeonyesha vyanzo vya mapato ya Neymar, unaonyesha ni jinsi gani nyota huyo wa Paris Saint-Germain ni mtambo wa kutegeneza fedha.

Hata hivyo, Gazeti la Marca la nchini humo limeeleza kuwa, Pamoja na kupokea euro 37 milioni kwa mwaka katika mshahara wake, nyota huyo wa Brazil kwa sasa anaingiza katika zaidi ya euro 459,000 kwa kila tangazo analotuma katika akaunti zake za Twitter, Instagram kwa mujibu wa utafiti wa Blinkfire.

“Kama ukichukua mambo yake yote aliyotuma katika akaunti zake za mitandao ya kijamii kwa Januari, inakadiliwa kufikia jumla ya thamani ya euro 34 milioni,” aliandika mkurungezi wa Blinkfire, Christian Olivares. “Kiasi hiko ndicho anachopaswa kuingiza kutokana na matangazo anayoweka hapo.”

Akaunti hizo zimeendelea kupata watu wengi wanaozifuatilia kila siku kwa sasa katika Instagram inawatu wanaoifuata 88.8 milioni, Facebook watu 60 milioni wakati katika Twitter anawatu 37.6 milioni.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s