Drogba, Eto’o watoa saluti kwa Mo Salah

Nyota wa zamani wa Afrika, Samuel Eto’o na Didier Drogba wamesema winga wa Liverpool, Mohamed Salah yupo kwenye anga moja la ubora na wakali Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

5a229537aabd42e52f000001

Salah yupo kwenye kiwango bora, akiwa amefunga mabao 21 kwenye Ligi Kuu England msimu huu kabla ya mechi ya jana na jambo hilo limewafanya mastaa wazamani waliowahi kushinda tuzo mchezaji bora ya mwaka ya Afrika, Drogba, Eto’o na El Hadji Diouf kusema naye ni bora miongoni mwa waliobora.

kwa mujibu wa Gazeti la The Sun, Eto’o alisema, “Ni wazi kabisa naye ni mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani. Kiwango chake cha Liverpool kuwa matata kabisa, kwangu mimi siku zote nafurahi ninapomwoona mchezaji wa Afrika yupo kwenye kiwango bora kabisa kama kile. Anastahi tuzo na naamini ataendelea kuwa hivi kwa miaka mingi zaidi.”

Staa wa Ivory Coast, Drogba alisema anachokiona ni kwamba Jurgen Klopp amekuwa kocha sahihi wa kumnoa Salah. Wakati walipokuwa pamoja Chelsea, Salah alishindwa kupata nafasi baada ya kocha Jose Mourinho kumwona kawaida tu.

Drogba, 39, alisema, “Siku zote amekuwa mchezaji mzuri. Sote tulifahamu kitu kilichopo ndani yake. Pengine kwa sasa amepata kocha anayempa nafasi na majukumu zaidi.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s